Vijana katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kutumia talanta zao kujipatia pato maishani.
Mkurugenzi wa shirika la vijana la Pwani Youth Network Alfred Sigo amesema kwamba vijana wa Pwani wana talanta nyingi japo wengi wao wamekosa kuzikuza ili ziwanufaishe maishani.
Akizungumza katika kongamano la vijana huko Mikindani kaunti ya Mombasa, Sigo amesema kwamba vijana wanapaswa kutumia talanta walizo nazo kujikwamua kiuchumi.
Sigo amewataka viongozi wa kaunti ya Mombasa kushirikiana na vijana na kuwashirikisha katika mikakati ya maendeleo mashinani akisema kwamba wakihusishwa kikamilifu uhalifu utadhibitiwa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni