Vijana katika maeneo ya Kisauni na Nyali katika kaunti ya Mombasa wametaka viongozi wa kaunti hiyo kuwekwa mipangilio mwafaka kuhusu swala la watu kutengwa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Vijana hao Wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Vijana la Kadzandani Creative, Omar Chai, wamesema wengi wao wanaogopa kupimwa kutokana na hali duni katika maeneo ambayo watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi hutengwa.
Chai amesema ni vyema iwapo mazingira katika maeneo hayo yataboreshwa zadii kabla ya wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuhimizwa kujitokeza kwa hiari ili kupimwa virusi hivyo.
Wakati uo huo, Chai amewataka wakaazi kujumuishwa kikamilifu katika mikakati ya hamasa kuhusu virusi hivyo kabla ya kupimwa.