Story by Gabriel Mwaganjoni –
Vijana katika kaunti ya Taita taveta wameshauriwa kutowategemea wanasiasa na badala yake kuwa wabunifu wa ajira kwani hali hiyo huwaweka vijana katika hali ya kupoteza matumaini.
Kiongozi wa vijana katika kaunti hiyo Robert Mwakumbaku amesema vijana wengi katika kaunti hiyo wameweka matumaini yao katika wanasiasa licha ya kuwa na uwezo wa kushirikiana na vijana wenzao na kuimarisha maisha yao.
Akizungumza mjini Voi, Mwakumbaku amesema kuwategemea wanasiasa kumewafanya vijana kukosa kujishughulisha katika maswala ya maendeleo.
Wakati uo huo, Mwanaharakati huyo wa vijana amedokeza kuwa ni sharti vijana wakumbatie elimu.