Vijana kutoka kaunti ya Kwale wamehamasishwa kuhusu umuhimu wa kudumumisha amani na jinsi ya kufikia haki zao , kwenye mkao uliowajumuisha maafisa wa serikali katika vitengo mbalimbali vya sheria.
Akiongea kwenye hafla hiyo iliyodhaminiwa na shirika la Search for Common Ground na mashirika mengine, meneja wa mipango katika shirika hilo Mohamed Ali Mwachausa, amesema kwamba lengo la mkao ni kuwakutanisha vijana na maafisa wa taasisi za sheria ili kuziba pengo lililoko kati ya makundi hayo mawili.
Mwachausa amesema kwamba kupitia mradi huo unaoendelezwa katika ukanda wa Pwani zaidi ya vijana 100 wamejinasua kutoka kwa makundi ya kihalifu na itikadi kali.
Mwachausa aidha amewahimiza maafisa wa usalama kujenga uhusiano mwema kati yao na vijana, ili kuimarisha uwiano na utangamano kwa manufaa ya kudumisha amani.
Taarifa na Michael Otieno.