Picha kwa hisani –
Vera Sidika na mpenzi wake Brown Mauzo wanazidi kuonyesha mapenzi mazito
katika mitandao ya kijamii kunoga kila uchao hata baada ya wengi kutabiri
kwamba wataachana baada ya muda mfupi.
Vera Sidika alitangaza kuchumbiwa na Mauzo mwezi jana siku ya kusherehekea
siku yake ya kuzaliwa huku hisia tofauti zikiibuka kupitia mtandao wa Instagram.
Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Sidika alimsifia mauzo
huku akisema kuwa ameolewa na rafiki wake wa dhati.
Niliolewa na rafiki yangu wa dhati, nakupenda sana mume
wangu @brownmauzo254 – Aliandika Vera.
Hata hivyo, baada ya mashabiki wake kuona ujumbe huo walifurika kwenye
mtandao huo na kuwapongeza kwa uhusiano wake mpya.