Picha Kwa Hisani – Vera Sidika Instagram Account
Mwanamitindo na mfanyabiashara Vera Sidika amefunguka kuhusu mipango ya kufunga harusi na mchumba wake Brown Mauzo. Vera amefichua hayo kupitia Insta stories.
Swala lake la kufunga ndoa na mwanamuziki huyo kutoka Mombasa ni jambo ambalo mashabiki wake wamekuwa wakiliuuliza mara kwa mara na mapema hii leo akaamua kumjibu mwanadada mmoja.
Vera alisema kwamba wanatazamia kufanya sherehe ya harusi baada ya janga la covid-19 kutoweka. Hii ni kutokana na kuwa alipendelea iwe sherehe ya kufana atakayo weza kuwaalika watu wengi.
Mwanamitindo huyo, amedumu kwenye mahusiano yake na mchumba wake ambaye ni mwanamuziki kutoka Mombasa, Brown, tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Pia aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Otile Brown na kuachana mwaka wa 2018.
Je, unahisi kuwa Vera Sidika alilijibu swali hilo kwa uzuri au kwa kinaya?