Picha kwa hisani –
Mwanasosholaiti na video vixen, Vera Sidika amezua gumzo baina ya mashabiki wake mitandaoni baada
ya kuposti picha akiwa nusu uchi huku akiwa amemshikilia mbwa na kifagio.
Vera ameonekana kutoshtuliwa na maneno ya wanamitandao kuhusu mavazi yake. Hapo awali kupitia
Instagram, alipakia picha kama hiyo huku wanamitandao wakimvalisha nguo kwa kutumia photoshoot,
lakini bado angalia anaendelea na mtindo huo.
Baada ya Vera kupakia picha hiyo aliandika ujumbe mfupi unaosoma, "Siku za jumamosi ni za kufanya usafi…kwa huduma yako."
Mashabiki wake walitoa hisia tofauti huku mmoja wa mashabiki wake wakimwambia kuwa yeye ndiye
kijakazi ghali zaidi ulimwenguni.