Hatimaye msanii Otile Brown ameweza kununua Benz ambayo Vera Sidika alidai kuwa alimkopa pesa ili aweze kununua.
Licha ya fanikio hilo kupokelewa vyema na mashabiki wa Otile, Kambi ya Vera imewaka moto baada ya mjarasiliamali huyo kudai kuwa gari hiyo imenunuliwa na pesa mtoto.
“Hongera kwa kununua Benz kwa bei ya saa yangu,” amebeza Verah huku akiambatanisha picha ya Otile akiwa na gari hilo.