
Mlimbwende Verah Sidika akiwa na Kendall Nicole Jenner. Picha/ Kwa hisani
Ikiwa ulidhani kuwa mwaka 2018 ndio ulikuwa mwaka wa Verah Sidika, umekosea pakubwa sana.
Mwaka huu bado ni mwaka wake.
Mlimbwende huyu ameuhakikishia ulimwengu kuwa bado yupo matawi ya juu baada ya kupiga unyunyu na walimbwende maarufu ulimwenguni “The Kardashians”.
Vera ambaye walipapurana na Otile Brown kwenye mitandao ya kijamii baada ya penzi lao kugeuka shubili aliweza kupitisha wakati wake na Kendal Nicole Jener, mmoja wa walimbwende katika familia hiyo tajiri ulimwenguni.
Wawili hao walikuwa pamoja wakati wa mechi ya mchezo wa kikapu kati ya LA Clippers dhidi ya Philadelphia 76ers.
Kama alivyowahi kutudhihirishia awali dalili zipo wazi kuwa biashara ipo kati ya “The Kardashians” na Vera Sidika.
Taarifa na Dominick Mwambui.