Timu ya Vanga United kutoka LungaLunga ndiyo mshindi wa mashindano ya Mama Kwale County Tournament iliyofikia katika uga wa shule ya upili ya Mwereni eneo bunge la Lungalunga baada ya kuichapa Lions FC kutoka Kinango bao 1-0 katika mikwaju ya penanti roundi ya pili.
Magwiji hao wawili walifungana bao 1-1 katika kipindi cha dakika 90 kabla ya kutoka 5-5 kwenye mikwaju ya penanti awamu ya Kwanza.
Mshindi wa Kwanza, Vanga United amejizoleaKsh 110,000 na kikombe nao washindi wa pili Lions FC wamejinyakulia Ksh 50,000 na mpira, mshindi wa tatu Kinango Raptors wametia kibindoni Ksh 30,000 pamoja na mpira na wa nne Ksh 10,000 na mpira.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni mwakilishi wa wadi ya Mackinnon Joseph Tsuma, Eliza Mjeni, Mwenyekiti wa NGAAF Omar Boga, Mshirikishi wa NGAAF Victor Nyanje na Muwakilishi wa Mbunge wa Kinango Richard Itambo miongoni mwa wengine.
Taarifa na Dominick Mwambui.