Mchekeshaji James Chanji Wamukoya maarufu kama Mshamba amemataka Rais Uhuru Kenyatta kuwaamurisha maofisaa wa polisi kuvaa Kanzu kama njia mojawapo ya kukabiliana na ufisadi.
Kulingana na Mshamba maofisaa wa polisi huweza kupokea hongo kwani magwanda yao yapo na mifuko mingi ya kuficha hongo.
Mchekesahaji huyo aliyezuru eneo la Pwani hivi majuzi amedai kuwa vita dhidi ya ufisadi humu nchini vinafaa kuzidishwa ili kuliokoa taifa kutoka kwa watu wachache walio na tamaa ya kupata mali.
Aidha amependekeza kufungwa mara moja kwa mtu atakayepatikana na hatia ya kuendeleza ufisadi.
Taarifa na Dominick Mwambui