Picha kwa hisani –
Ulimwengu hii leo unaadhimisha siku ya wapendanao duniani, siku ambayo inaashiria upendo na ujamaa baina ya watu walio katika mahusiano na jamii.
Siku hii huadhimishwa kote ulimwenguni kwa aina tofauti huku wengine wakivalia mavazi ya rangi nyekundu sawia na kubeba mau ya rangi sawia na hiyo ishara ya kuonyesha upendo.
Watu wa tabaka mbalimbali hutembelea na kusheherekea siku hii hasa wale walio katika mahusiano kuonyesha upendo na pamoja na familia husherekea siku hii.