Picha Kwa Hisani
Shirika la huduma za misitu nchini KFS kwa ushirikiano na baraza la kitaifa la vijana wamezindua upanzi wa miche 600 katika njia moja wapo ya kudhibiti mazingira.
Akizungumza wakati wa halfa ya maadhimisho ya siku ya Mazingira ulimwenguni yaliandaliwa katika kaunti ya Kwale, Meneja wa Shirika hilo katika kituo cha Kwale Edwin Misache zoezi hilo litaendelea ili kuafikia azmio la asilimia 10 la misitu mwaka wa 2022.
Misache amesema hatua hiyo itahakikisha misitu ya humu nchini itaboreshwa zaidi na katika mzingira salama ili kuhakisha misiti inalindwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa baraza la kitaifa la vijana Sasaka Telewa amewahimiza vijana kukupambatia upanzi wa miti hususan miti ya matunda ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa chakula.