Picha Kwa Hisani – Trio Mio’s Instagram Account
Msanii wa Genge Tone Trio Mio mwenye umri wa miaka 16, amepakia picha akiwa amevaa sare ya shule kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuchapisha ujumbe akiwaeleza mashabiki wake kuwa anarudi shule na pia atawakosa Sana.
Ni mwanamuziki anayezidi kutamba mitandaoni baada ya uwezo wake kwenye Sanaa ya muziki kulinganishwa na ya marehemu E-Sir alipokuwa hai.
Siku ya Jana, wanamuziki wengi akiwemo mkongwe wa sanaa nchini Nameless pamoja na wanamitandao walijitokeza na kumpongeza Trio kwa kipaji chake.
Trio Mio anaendelea kuvuma kwa remix ya ngoma yake ‘Cheza kama wewe’ aliyoimba na mwanamuzikiMejja wa utawezana, Exraay pamoja na Nellythegoon ambao kufikia sasa umetazamwa na watu zaidi ya milioni 6 kwenye mtandao wake wa YouTube.
Aidha, wengine walitoa maoni tofauti na kusema kuwa ingawa ana talanta lakini hakupaswa kufananishwa na Esir.