Utumizi wa mihadarati miongoni mwa wanafunzi wenye umri mdogo umetajwa kuwa tatizo kubwa katika shule za msingi na upili katika eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Mwalimu wa kitengo kinachoangazia maslahi ya wanafunzi katika shule ya msingi ya Mtomondoni Moses Kombero, baadhi ya wanafunzi wenye umri mdogo wanatumia dawa za kulevya.
Akizungumza shuleni humo, Kombero amesema hali hiyo inastahili kudhibitiwa mapema akisema tayari jitihada za kuikabili hali hiyo zinaendelezwa.
Kombero hata hivyo amesema kuwa utumizi huo umedhibitiwa akiwataka wadau wakiwemo Wazazi, Viongozi wa kidini na wa kijamii na Wasimamizi wa shule mbalimbali eneo hilo kujitahidi zaidi kukomesha kabisa utumizi wa mihadarati.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.