Picha kwa hisani –
Baraza la almashauri ya kiislamu nchini KEMNAC limetilia shaka uteuzi wa Kadhi mkuu nchini likisema uteuzi huo unatekelezwa kiubaguzi.
Katika taarifa yake kwa wanabari hapo jana mwenyekiti wa Baraza hilo Sheikh Juma Ngao ameitaka Tume ya huduma za mahakama nchini JSC kuhakikisha uchaguzi wa Kadhi mkuu unajumuisha jamii zote.
Sheikh Ngao amefichua kuwa baraza hilo litakuwa macho na kufuatilia kwa karibu shughuli zote na misaada inayotumwa humu nchini ili kuikimu jamii ya kiislamu.
Wadhfa huo kwa sasa unashikiliwa na kadhi mkuu Sheikh Shariff Ahmed Muhdhar.