Utata kuhusu sikukuu ya Eid – Ul – Adh’Ha umezidi mjini Mombasa baada ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kuungana kusali sala yao ya Eid- Ul- Adh’ Ha katika uwanja wa Tononoka mjini Mombasa.
Haya yanajiri huku kundi jingine la waumini hao wakipanga maombo hapo kesho.
Kwa upande wake Imam wa msikiti wa Ibrahims eneo la Ganjoni kaunti ya Mombasa Abu Qattada ni kuwa kuwa leo ndio siku ya sikukuu kulingana na waumini waliokwenda Hijjah katika mji wa Mekkah licha Kadhi mkuu nchini kutangaza sala hiyo kusaliwa kesho.
Katibu mtendaji wa baraza la Maimamu na Wahubiri humu nchini, Mohammed Khalif amewahimiza wale walioaajaaliwa kuchinja kugawia wale ambao hawana uwezo.