Utata umeghubika maadhimisho ya siku kuu ya Eid-ul- Adha baada ya baadhi ya waumini kusherehekea leo badala ya kesho alivyoagiza kadhi mkuu nchini Ahmed Muhdhar.
Waumini hao wamemiminika katika misikiti na viwanja mbali mbali kwa swala hiyo maalum ya Eid- ul- Adha.
Mjini Mombasa katibu mtendaji wa baraza la maimamu na wahubiri wa humu nchini Sheikh Mohhamed Khalifa ameongoza mamia ya waumini kwa swala hiyo maalum ya EID –UL –ADHA.
Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilika kwa swala hiyo sheikh Khalifa amewaomba wananchi kudumisha uwiano.
Kwa upande wake Sheikh Abu Qatada wa msikiti musa ulioko eneo la majengo mjini Mombasa amewahimiza waumini waislamu kuwakumbuka wasiojiweza na wale wasiobahatika katika jamii.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.