Picha kwa hisani –
Katibu mkuu wa baraza la walimu wa madrasa katika kaunti ya Kilifi, Ustadh Athman Said amesema kufikia sasa wasimamizi wa misikiti katika kaunti hiyo wameekeza mikakati ya kuhakikisha waumini wanazingatia sheria za kuzuia maambukizi ya corona.
Akizungumza mjini Malindi hapo jana, Ustadh Athman amekariri kuwa makali ya janga la Corona yanaendelea kushuhudiwa na kuna haja ya wakaazi kutopuuza masharti yaliotolewa na serikali ili kujikinga na maradhi hayo.
Hata hivyo amewahimiza waumini wa dini mbalimbali nchini kuhakikisha wanazingatia masharti ya kiafya, akisema afya ya kila mmoja ni muhimu kwa taifa hili.