Story by Our Correspondents-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeweka wazi kwamba haitawalipa marupurupu maafisa wa usalama watakaoshika doria wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Katibu katika Wizara ya Usalama wa ndani Karanja Kibicho, amesema hatua hiyo ya IEBC inaungwa mkono kikamilifu na serikali kwani tayari Wizara ya usalama nchini imetanga bajeti kwa ajali ya marupurupu hayo ya maafisa wa usalama.
Kibicho amedokeza kwamba Wizara ya usalama itawatuma maafisa wa usalama laki moja kutoka vitengo mbalimbali vya usalama nchini ili kushirika doria kikamilifu wakati wa uchaguzi mkuu.
Wakati uo huo amewasihi maafisa wa usalama nchini ikiwemo machifu na manaibu wao kuhakikisha wanasisitiza umuhimu wa amani kote nchini kuanzia mashinani.