Story by Janet Shume –
Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Ambrose Oloo ametoa onyo kali kwa wazazi wa kaunti hiyo dhidi ya kuwapa uhuru wa kupindukia watoto wao wakati wa sikukuu ya Eid-ul-Fitr.
Oloo amesema wazazi wanapaswa kuchukua jukumu la kuwalinda watoto wao kipindi chote cha shamra shamra ili kuhakikisha kwamba wako salama.
Kamanda huyo wa polisi kaunti ya Kwale ametoa hakikisho kwamba maafisa wa polisi watazidisha doria kila eneo la kaunti hiyo ili kuhakikisha usalama unaimarishwa.
Wakati uo huo amewapongeza waumini wa dini ya kiislamu katika kaunti ya Kwale kwa kuzingatia maagizo yaliyowekwa na Wizara ya Afya nchini ya kudhibiti janga la Corona akisema idara ya usalama itaweka mazingira bora kuhakikisha waumini wa dini ya kiislamu wanasherehea kwa amani.