Idara ya usalama kaunti ya Kwale imedai kuwa usalama utaimarishwa kikamilifu katika kila eneo ili kuhakikisha visa vya utovu wa usalama havishuhudiwa wakati huu ambapo taifa linakabiliana na janga la Corona.
Afisa mkuu wa polisi eneo la Matuga Francis Nguli amesema maafisa wa polisi wa kutosha watatumwa nyanjani kuhakikisha hakuna visa vyovyote vya utovu wa vinashuhudiwa.
Katika swala la magari ya uchukuzi wa umma, afisa huyo wa polisi amesema abiria watakaokaidi agizo la serikali la kukuabiri magari ya umma wakiwa kidogo watachukuliwa hatua.