Shughuli za masomo na zile za kibiashara zimetatizika huku familia kadhaa zikiachwa bila makao baada ya majengo yao kuharibiwa na upepo mkali katika kijiji cha chakama eneo la Malindi kaunti ya Kilifi.
Akizungumzia tukio hilo mwalimu mkuu wa shule ya Matolani Lucas Deche amesema kuwa paa za shule kadhaa katika eneo hilo zimesombwa na upeo mkali sawa na vifaa vyengine vya kielektroniki na kusababisha hasara kubwa.
Chifu wa eneo hilo Solomon Mbashiri amethibitisha mkasa huo akisema kuwa kimbunga hicho kimesababishwa na mvua kali ilionyesha kwa takriban nusu saa.
Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu wamefika eneo la tukio kutathmini hasara waliopata wakaazi.
Taarifa na Charo Banda.