Picha Kwa Hisani
Mwili wa kijana anayedaiwa kufariki katika kituo cha polisi cha Kijipwa kule Vipingo kaunti ya Kilifi umefanyiwa upasuaji katika hospitali kuu ya Kilifi.
Wakizungumza na Wanahabari baada ya kushuhudia upasuaji wa mwili huo,hapo jana Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yakiongonzwa na Shirika la Haki Afrika yamesema kifo cha kijana huyo kilichangiwa na kukosa hewa.
Kulingana na Afisa wa Shirika la Haki Africa Harriet Muganda, visa vya watu kujinyonga katika vituo vya polisi katika kaunti ya Kilifi vimekithiri na kuwataka maafisa wa usalama kuchunguzwa.
Kwa upande wake mmoja wa familia ya Marehemu Samson Chege amesema kwa sasa familia haijafanya uamuzi wowote kuhusiana na ripoti ya upasuaji ya mwendazake.
Kijana huyo alifariki siku ya Jumanne usiku wiki iliopita katika kituo cha polisi cha Kijipwa kule Vipingo kaunti ya Kilifi katika mazingira tata.