Siku chache tu baada ya Idara ya Elimu gatuzi ndogo la Malindi kuifunga shule ya upili ya Wavulana ya Tahweed, sasa usimamizi wa shule hiyo pamoja na wazazi wamejitokeza na kulaani vikali hatua hiyo.
Akizungumza na Wanahabari mjini Malindi, Mkurungenzi mkuu wa shule hiyo Amri Ahmed Mjaa, amepuuzilia mbali madai ya shule hiyo kutokuwa na stakabadhi za kuoyesha kuwa shule hiyo imesajiliwa.
Amri ameitaja hatua hiyo kama kinyume cha sheria, akisema shule hiyo ilipata kibali cha usajili mnamo mwaka wa 2014.
Amri amedai kuwa idara ya elimu haikuchunguza kwa undani jinsi shule hiyo inavyoendesha shuhuli zake huku akisema Mkurugenzi mkuu Idara ya elimu eneo la Malindi anatumia mamlaka yake vibaya.
Taarifa Charo Banda.