Picha kwa Hisani –
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kuzuia watu kujitoa uhai,umoja wa mataifa umetaka mashirika na watu binafsi kuendeleza hamasa kwa umma kuhusu jinsi ya kukabili matatizo ya kiakili yanayopelekea watu kujitoa uhai.
Katika ujumbe wake kuhusu maadhimisho haya umoja wa mataifa umesema watu elfu 3 uaga dunia kila siku kote ulimwenguni kupitia kujitoa uhai huku watu milioni moja wakifariki kwa kujitoa uhai kila mwaka.
Umoja wa mataifa vile vile umesema kujitoa uhai kumechangia vifo vya watu wengi wakiwa na umri mdogo na kwamba kuna haja ya jamii kuungana kumaliza matatizo yanayochangia watu kujitoa uhai.
Maadhimisho haya yanaendelezwa huku visa vya watu kujitoa uhai humu nchini vikitajwa kuongezeka.