Picha kwa Hisani –
Ulimwengu hii leo unaendelea kuadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa sauti yangu usawa wetu wa baadaye.
Umoja wa mataifa umeyahimiza mataifa ya wanachama kuhakikisha yanatambua umuhimu wa mtoto wa kike, na kuziakabilia changamoto zinazowasibu.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Gutteres katika ujumbe wake kwa mataifa wanachama, amesema umoja wa mataifa unaendeleza mikakati ya kuhakikisha ulimwengu unabuni mbinu za kuwalinda watoto wa kike.
Nchini Kenya, Shirika la Plan International, limesema idadi kubwa ya wasichana wameonekana kupitia unyanyasaji wa hali ya juu ikiwemo dhulma za kijinsia na kingono bila ya usaidizi wowote.
Shirika hilo hata hivyo limehimiza serikali ya kitaifa na zile za kaunti kuibuka na mikakati itakayowalinda watoto wa kike dhidi ya maovu.