Picha kwa Hisani
Kenya imeungana na mataifa mengine yaliowanachama wa umoja wa mataifa kuadhimisha siku ya kupambana na ugonjwa wa homa ya ini yaani hepatitis.
Katika ujumbe wake kuhusu maadhimisho ya mwaka huu shirika la afya duniani WHO limeyataka mataifa kuchukua hatua za dharura kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kutoka kwa mama hadi kwa mtoto,sawa na kuhakikisha wanaopata ugonjwa huo wanapata tiba.
WHO imesema aina za Hepatitis B na C ndio hatari zaidi na usababisha takriban asilimia 80 ya vifo vyote vya saratani ya ini na kuuwa watu milioni 1.4 kwa mwaka.
Shirika hilo limesema kipindi hiki cha janga la Corona ugonjwa huo wa homa ya ini yaani Hepatitis unasababisha vifo vya watu wengi kwa siku ulimwenguni.