Picha kwa hisani –
Kenya hii leo inajiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya mama.
Siku hii huadhimishwa kila mwaka kushinikiza mataifa mbalimbali ulimwenguni kuenzi lugha ya mama na kuhakikisha lugha ya mama haitokomezwi ili kufanikisha maendeleo ya pamoja.
Kwa mujibu wa shirika la elimu, Sayansi na Utamadini la Umoja wa Mataifa UNESCO, kati ya lugha 6,000 za mama duniani, asilimia 50 kati yao ziko katika hatari ya kuangamia.
Utunzi wa lugha za mama umekuwa pia changamoto kwa maendeleo licha ya lugha kuwa ni kiungo muhimu ya kupitisha ujumbe na pia ni kitu ambacho hakitarudiwa tena ikiwa itatoweka.