Picha kwa hisani –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i amesema serikali itachapisha majina ya wale wanaoshukiwa kuwa walanguzi wakuu wa dawa za kulevya na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza na Wanahabari kule Mombasa baada ya kufanya ziara ya kiusalama na kukagua miradi ya maendeleo ya serikali, Waziri Matiang’i amesema ulanguzi wa dawa za kulevya umechangia pakubwa utovu wa usalama.
Waziri Matiang’i amesema serikali haiwezi kukubali kuona idadi kubwa ya vijana wakioangamia kutokana na makali ya dawa za kulevya huku baadhi ya watu wakiendeleza kutengeza fedha kupitia biashara hiyo haramu.
Kauli yake imejiri baada ya watu wanne kutiwa nguvuni kule Mombasa kwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroine na Cocaine zenye thamani ya shilingi milioni 6.