Waziri wa Michezo, Utamaduni na Turathi za kitaifa Balozi Amina Mohammed amesema ameridhishwa na ujenzi wa ukuta katika ngome ya kitaifa ya Fort Jesus Mjini Mombasa.
Ujenzi huo unalenga kuzuia makavazi hayo ya kitaifa kuliwa na Bahari hindi.
Kulingana na Amina, ujenzi huo umefanyika kulingana na mipangilio na utazuia kumomonyoka kwa Makavazi hayo ya kitaifa ambao yalikuwa katika hatari na kuliwa na Bahari hindi na hatimaye kubomoka kabisa.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Bi Mohammed amesema kwamba tayari Idara ya makavazi ya kitaifa nchini imekabidhiwa cheti cha kukamilika kwa ujenzi huo akisema kwamba vile vile litaboreshwa na kuwa eneo la Wakaazi na wageni kujivinjari.
Amehoji kwamba huenda ujenzi huo ukapanuliwa zaidi hadi katika upande wa hospitali ya kibinafsi ya Mombasa yaani ‘Mombasa hospital’ inayoshikana na ngome hiyo ya kitaifa ya Fort Jesus.