Pika kwa Hisani –
Waziri wa fedha nchini Ukur Yattani ameongoza hafla ya kutia saini mkataba wa makubaliano wa kuunganisha halmashauri ya bandari nchini KPA,kampuni ya kusambaza mafuta KPC na shirika la reli nchini.
Akizungumza wakati wa hafla hio katika bandari ya Mombasa Yattani amesema taasisi hizo ambazo sasa ni shirika moja ziko chini ya mamlaka ya uchukuzi ya ‘Kenya Transport and Logistic Network’ (KTLN).
Yattani amesema kuwa kuunganishwa kwa mashirika hayo matatu kunalenga kuimarisha utendakazi wa mashirika hayo kwani yatakua na uwezo wa kutumia rasilimali zao pamoja.
Kwa upande wake katibu katika wizara ya madini na mafuta anaesimamia idara ya mafuta (Department of petroleum) Andrew Kamau amesema kuunganishwa kwa mashirika hayo ni hatua kubwa kwa taifa hili na kutapelekea kuimarika zaidi kwa uchumi wa taifa
Naye Bi Wanjiku Koge aliezungumza kwa niaba ya mkuu wa huduma za umma nchini Joseph Kinyua,amesema muungano huo utasaidia kupunguza ada za kuendeleza biashara kwa mashirika hayo.
Kutiwa saini kwa mkataba huo kumejiri baada ya rais Uhuru Kenyatta mapema mwezi agosti kutia saini agozp la kutaka mashirika hayo matatu yaunganishwe ambapo aliipa mamlaka wizara ya fedha kuwa muangalizi wa taasisi hio mpya ya KTLN.