Picha Kwa Hisani –
Waziri wa fedha nchini Ukur Yattani amesema hatua ya maseneta kutoafikiana kuhusu mfumo wa ugavi wa fedha kwa kaunti inarudisha nyuma taifa hili kiuchumi.
Akizungumza jijini Nairobi Yattani amesema kaunti za humu nchini zinahitaji rasilimali ili kuendeleza shughuli zake ikiwemo zile za maendeleo ambazo uchangia pato kwa taifa.
Yattani amesema wizara ya fedha haina mamlaka kusambaza fedha kwa kaunti za humu nchini hadi pale maseneta watakapoafikiana kuhusu mfumo muafaka wa ugavi wa mapato.
Waziri huyo wa fedha nchini amewataka maseneta kuafikiana mara moja ili kuhakikisha kaunti zinapata fedha za kuendeleza miradi itakayowanufaisha wananchi.