Huenda ukulima wa mnazi hapa Pwani ukaimarika zaidi, iwapo mradi wa majaribio ya mbegu ya kisasa yaani Hybrid utafanikiwa.
Akiongea katika eneo la Matuga kaunti ya Kwale wakati wa uzinduzi wa miche 2,131 ya mbegu za kisasa za mmea wa mnazi, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa Kilimo na mifugo nchini Daktari Eliud Kereger, amesema mradi huo unapania kuinua mapato ya wakulima wa mnazi.
Kereger amesema mradi huo wa majaribio unawalenga wakulima 21 kutoka kaunti tatu za Pwani, ikiwemo Kwale, Kilifi na taita Taveta, ili kila mkulima apate miche 32.
Kwa pande wake Mwakilishi wa Katibu katika Wizara ya Kilimo na ufugaji Jane Otado, amezihimiza serikali za kaunti hizo tatu kushirikiana na Wizara ya Kilimo ili kufanikisha mradi huo.
Taarifa na Salim Mwakazi.