Story by Ali Chete –
Ukosefu wa vyanzo vya uzalishaji maji katika kaunti ya Mombasa ndio chanzo kikuu cha uhaba wa maji katika kaunti hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji maji ya Mombasa Abdulrahim Farah amasema kaunti ya Mombasa imetegemea kaunti jirani za Kilifi, Kwale na Taita Taveta kupata huduma hiyo bora ya maji.
Akizungumza na katika kaunti ya Mombasa wakati wa maadhimisho ya siku ya maji duniani, mkurugenzi huyo amehoji kuwa serikali kuu pamoja na serikali ya kaunti ya Mombasa imeweka mikakakti ambayo itakomesha uhaba huo unaoikumba kaunti hiyo.
Wakati uo huo amedokeza kuwa kufuatia idadi kubwa ya watu wanaoishi katika kaunti hiyo na wale anaotembelea kaunti hiyo kama watalii wamelazimika kusambaza bidhaa hiyo muhimu kwa zamu katika maeneo tofauti tofauti ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya wakaazi wa kaunti hiyo.