Story by Janet Shume –
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Yetu linaendeleza hamasa kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia vinavyoendelea kukithiri katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale.
Akizungumza na wakaazi wa Ndavaya, Afisa wa Shirika hilo Munira Abubakar amesema kesi nyingi za dhulma za kijinsia zimekuwa zikichukua muda mrefu kutatuliwa Mahakama kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.
Kwa upande wake Afisa wa watoto eneo bunge hilo Monica Ndaro amewataka wakaazi wa eneo hilo kuzingatia ushahidi wa visa hivyo pindi vinapotokea, akisema hatua hiyo itahakikisha wahusika wote wanachukuliwa hatua.
Hata hivyo ameitaka idara ya Mahakama hususan mjini Kwale kuweka kipaumbele kesi zinazohusiana na dhulma za watoto ili waathiriwa wapate haki.