Mwanzilishi wa wakfu wa Kitaka, Ali Kitaka amesema kuwa idadi kubwa ya vijana Likoni wanajihusisha na uhalifu kwa kukosa njia za kujiendeleza maishani.
Akiongea huko Likoni Kitaka amehoji kwamba visa vya uhalifu eneo hilo vitapungua ikiwa vijana watakuzwa kitalanta na kuwezeshwa kujitegemea kupitia talanta.
Kitaka amesema kupitia kwa wakfu wake atahakikisha vijana wanajinasua kwa utumizi wa mihadarati na kusaidiwa kukuza talanta zao mbali mbali.
Mdau huyo amehimiza ushirikiano wa wananchi na idara ya usalama kuwanasua vijana kutoka kwa uhalifu.
Taarifa na Hussein Mdune.