Katibu mtendaji wa Baraza la Maimam na wahubiri wa humu nchini CIPK, Sheikh Mohammed Khalifa amesema ukosefu wa hamasa kuhusu ukadiriaji wa bajeti umechangia pakubwa kupanda kwa gharama ya maisha.
Sheikh Khalifa amesisitiza umuhimu wa vikao vya hamasa kuandaliwa kabla ya mambo muhimu yanayomhusu mwanachi kuidhinishwa kwani hatua hiyo ndio imechangia kuwepo kwa changamoto nyingi.
Sheikh Khalifa amesema serikali ya kaunti ya Mombasa imekosa ushirikiano mwema baina yao na wananchi na kuchangia uadui mkubwa kwa kuwanyanyasa wananchi kupitia ushuru wa hali ya juu.
Kwa upande wake Waziri wa Ugatuzi katika kaunti ya Mombasa Seth Odogo amedai kuwa serikali ya kaunti hiyo inajizatiti katika kufanikisha ushirikiana bora baina yao na wakaazi ili kupiga hatua kimaendeleo.
Taarifa na Hussein Mdune.