Picha Kwa Hisani
Ni wazi kwamba mwanamuziki kutoka Pwani Nyota Ndogo anapitia kipindi kigumu cha maisha haswa kwenye ndoa yake.
Hii ni baada ya mume wake Hunning Neilsen kukata mawasiliano kwa muda wa mwezi na nusu sasa kwa kile Nyota anachodai kuwa mzaha.
Kulingana na mwanamuziki huyo, hajaweza kuwasiliana na Hunning tangu siku ya April Fools alipomfanyia matani kuwa amebeba ujauzito.
Baada ya majaribio ya kuomba msamaha na kumwomba mume wake amrudie, kwa kupost zaidi ya siku tatu mtawalia, sasa mashabiki wa mwanamuziki huyo wamejitokeza na kumshauri asonge mbele na maisha yake.
Waliongeza kuwa alikuwa anamtafutia sababu tu kwani mzaha tu hauwezi kumfukuza mtu aliye na mapenzi ya dhati.
Je, una ushauri upi kwa Nyota Ndogo kuhusiana na swala hili?