Picha kwa hisani –
Kinara wa chama cha NARC Kenya Bi Martha Karua amesema ukandamizaji wa demokrasia unaoshuhudiwa humu nchini unalirudisha nyuma taifa hili kimaendeleo.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Bi Karua ametaka viongozi wakuu serikali kuzingatia katiba ya nchini katika utendakazi wao hasa vipengele vinavyoangazia masuala demokrasia.
Karua amewataka wakenya kuungana kuipinga ripoti ya jopo la maridhiano ya BBI ambayo anadai kwamba inalenga kuwanufaisha watu wachache.