Story by Ngombo Jeff –
Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro amesema kuna haja ya viongozi nchini na wale wa kaunti kuibuni na mbinu mbadala za kujengwa viwanda vya nguo ili kutoa nafasi za ajira kwa vijana.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa katika kaunti ya Kilifi, Mung’aro amesema viwanda hivyo vitaajiri zaidi ya vijana elfu kumi katika kila eneo bunge la kaunti iwapo viongozi watawekeza zaidi swala hilo.
Kiongozi huyo amedokeza kwamba mpango huo unalenga kuwainua kiuchumi wakaazi wengi sawa na kuzikabili changamoto mbalimbali mashinani.
Wakati uo huo ameahidi kuzikabilia changamoto za uhaba wa maji iwapo wananchi wa kaunti ya Kilifi watamchangua kama kiongozi wao.