Mwenyekiti wa makundi ya watu wanaoishi na ulemavu kanda ya pwani Bi Hamisa Zajja amesema kuwa ukosefu wa ushirikiano kati ya maafisa wa polisi na wanajamii katika maeneo ya mashinani kumechangia pakubwa kudorora kwa usalama hapa Pwani.
Akiongea mjini Mombasa Bi Zajja amesema idara ya usalama pwani inafaa kushirikiana kikamilifu na wakaazi iwapo inalenga kumaliza tatizo hilo,kwani wanafahamu vyema vyanzo vya wahalifu.
Aidha amewasihi wazazi kuwafundisha maadili mema watoto wao ili wasijiunge na uhalifu.
Taarifa na Hussein Mdune.