Naibu wa rais William Ruto mapema leo ameungana na bodi ya huduma za maji kanda ya pwani na kuidhinisha tanki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya lita milioni 5 za maji katika eneo la mabirikani kaunti ya Kilifi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Ruto amesema hatua hio ni mbinu moja wapo ya kuboresha huduma za usambazaji maji kanda ya pwani na itakabili uhaba wa maji unaoshuhudiwa mara kwa mara.
Ruto vile vile amefichua kwamba fedha zilizotolewa kwenye mkataba wa maji kati ya kaunti za pwani na benki ya dunia zitaanza kutumika rasmi mwezi huu wa septemba ili kuhakikisha huduma za maji zinafika hadi mashinani.
Mwenyekiti Wa bodi ya maji pwani Mustafa Iddi amesema bodi hio itazidisha ushirikiano wake na serikali ya kaunti ya Kilifi katika kuhakikisha ubaha wa maji katika kaunti hio unasuluhishwa.