Uhaba wa madarasa, Madawati na Vyoo ndio chanzo cha elimu duni katika baadhi ya shule za eneo bunge la Rabai kule kaunti ya Kilifi.
Changamoto hiyo imebaika wakati wa ziara ya Mbunge wa eneo hilo William Kamoti katika shule za Secondari na msingi.
Akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika shule ya upili ya Rabai, Kamoti amesema kuna haja ya suala hilo kushuhulikiwa kwa wakati ili kuwawezesha wanafunzi wa shule hizo kusomea katika mazingira masafi.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Rabai Anderson Munga ameelezea changamoto wanaozpitia wanafunzi katika shule hiyo, akiwaomba wahisi kujitokeza na kuwasaidia kuboresha elimu.
Taarifa na Mercy Tumaini.