Story by Our Correspondent:
Waziri wa nishati wa Uganda Ruth Nankabirwa amesema nchi hiyo inafanya mazungumzo na Tanzania ili kusafirisha bidhaa zake zote za mafuta kupitia bandari ya Dar es Salaam.
Hii ina maanisha kwamba serikali ya Uganda haitatumia tena bandari ya Mombasa nchini Kenya iwapo mazungumzo hayo yataafikiwa.
Uganda haijaridhishwa na mfumo wa muda mrefu ambao kampuni za mafuta za Uganda zimekuwa zikinunua bidhaa zao kupitia kampuni tanzu za Kenya kwa asilimia 90.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akilalamika kuhusu usumbufu wa soko la mafuta na bei za juu za mafuta kupitia bandari ya Mombasa.