Idara ya usalama kanda ya Pwani imesema uchuguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto ulizuka katika hospitali ya kibinafsi ya Mombasa hospital.
Kamanda wa Polisi kanda ya Pwani Rashid Yakub, amesema japo tetesi zinaenezwa kuwa moto huo ulichangiwa na mlipoko wa mtungi wa gesi katika sehemu ya jikoni mwa hospitali hiyo, uchunguzi unaendelea.
Yakub amesema tayari usimamizi wa hospitali hiyo wamekubali kuifunga hospitali hiyo kwa muda usiojulikana, akisema wagonjwa 68 waliokuwa katika hospitali hiyo wamehamishiwa katika hospitali mbalimbali kwa matibabu.