Picha kwa hisani –
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amesema uchumi wa kaunti ya Kilifi umeathirika pakubwa kufuatia kuporomoka kwa sekta ya utalii, mjini Malindi.
Akizungumza nyumbani kwake huko Kakuyuni, mbunge huyo amesema hali hiyo imechangiwa na kupungua kwa idadi ya wageni wanaozuru eneo hilo, kutokana na mazingira duni mjini humo, hatua iliyopelekea hoteli nyingi kufungwa kwa kukosa wageni.
Kulingana na kiongozi huyo ameitaka serikali ya kaunti hio kubuni mikakati ambayo itasaidia sekta ya utalii kuimarika, ili kuokoa maisha ya wakazi wa sehemu hiyo, ambao wengi wamesalia bila ajira baada ya hoteli nyingi kufungwa.
Hata hivyo Jumwa amedokeza kuwa serikali hiyo ya kaunti, inapaswa kufanya kila iwezalo ili kuhakikisha uchumi wa Malindi ndio uti wa mgongo wa uchumi wa kaunti hiyo.
Wakati huo huo mbunge huyo ameelezea haja ya kuboreshwa kwa mazingira ya mji huo, ili kuweza kuwavutia watalii zaidi.