Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake wanaopambana na ugonjwa maradhi ya akili katika kaunti ya Mombasa la ‘Mombasa Women Empowerment Network’ Amina Abdallah amesema janga la Corona na uchumi duni miongoni mwa wakaazi wa kaunti hiyo kumechangia baadhi yao kuugua maradhi ya akili.
Amina amesema ongezeko hilo la watu wenye akili taahira katika kaunti ya Mombasa kumewasukuma wanawake hao kuanza kuwachukua waathiriwa hao na kuwapeleka katika taasisi maalum ya matibabu.
Mwanaharakati huyo wa Wanawake katika kaunti ya Mombasa amesema juhudi hizo zitasaidia katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona sio tu kwa wagonjwa hao bali pia wakaazi wengine wa kaunti hiyo.
Kwa upande wake, Florence Ojode wamekiri kwamba eneo la Utange kule Kisauni linashuhudia ongezeko la watu wanaougua maradhi ya akili.