Kwa mara ya kwanza katika historia tuzo za wanaspoti bora nchini soya zitaandaliwa nje ya jiji la Nairobi.
Hii ni baadaya mwanzilishi wa tuzo hizo Paul Tergat kutia saini mkataba wa maelewano na serikali ya kaunti ya Mombasa kuandaa makala ya 15 ya tuzo hizo katika kaunti hiyo.
Akizungumza baadaya kutia saini mkataba wa maelewano na Gavana wa Mombasa Hassan Joho katika afisi zake Tergat amesema kuwa yuko tayari kuzuru maeneo tofauti tofauti nchini kuinua na kukuza talanta za vijana wachanaga huku akiwahimiza wadau wa sekta mbalimbali kujitokeza na kuwekeza katika ukuzaji wa michezo nchini.
kwa upande wake Gavana Joho amedokeza kuwa kuandaliwa kwa tuzo hizo katika kaunti ya Mombasa kutawapa motisha zaidi vijana wa kaunti hiyo kujikuza kisporti.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.