Picha kwa hisani –
Kamishna wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka amewaonya walanguzi wa dawa za kulevya katika kaunti hiyo kwamba idara ya usalama imejipanga kuwakabili.
Olaka amesema idara ya usalama imeidhinisha mikakati maalum ya kuhakikisha wanaoendeleza biashara hiyo haramu watatiwa nguvuni na kufunguliwa mashtaka akiyataja maeneo ya mtwapa na Kilifi kama yaliosheheni biashara hio.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la vijana wa kiisalma la Kenya Muslim Youth Alliance tawi la kaunti ya Kilifi Muhamud Hambal amesema idadi kubwa ya watumizi wa mihadarati katika kaunti hiyo ni vijana wenye umri mdogo.